• Skip to content
  • Skip to primary sidebar
  • Skip to footer
  • Nyumbani
  • App ya Redio Uhai
  • Podikasiti
  • Radio Uhai Podikasiti
  • Rasilimali za Kikristo
  • Duka Le Redio Uhai
  • Mwongozo wa Vipindi
  • Wasiliana Nasi
  • Sikiliza kwa njia ya Mtandao
  • Angalia kwa Mtandao
  • Changia Redio Uhai Ukiwa Nje Ya Nchi
  • Changia Redio Uhai Ukiwa Tanzania
  • Habari Za Tanzania
  • Habari Za Kimataifa
  • Habari za Michezo
  • Paypal

Radio Uhai

Sauti Ya Tumaini

Habari Kitaifa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi ashikiliwa na Jeshi la Polisi

February 5, 2019 By

Watu watano, akiwamo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi, Pius Luhende, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida, wakituhumiwa kusababisha kifo cha mfugaji Peter Chambalo, anayedaiwa kupigwa risasi akiwa kanisani.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Ahmed Msangi, amesema tukio hilo limetokea juzi na kueleza kuwa mpaka sasa, wanaoshikiliwa ni watu  watano akiwamo mkurugenzi huyo.

Msangi amewataja watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni askari wanyamapori wawili, mmoja kutoka Mamlaka ya Wanyamapori (Tawa) na mwingine kutoka Halmashauri ya Ipigi, mwanasheria na mtendaji wa kata.

Ameongeza kuwa, wakati wa vurugu hizo, inadaiwa askari walifyatua risasi na kumjeruhi mtu huyo ambaye alifariki dunia.

Filed Under: Habari Kitaifa

Spika wa Bunge ameiagiza Serikali kutoa kauli kuhusu mauaji ya watoto

February 5, 2019 By

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameiagiza Serikali kutoa kauli kuhusu mauaji ya watoto yanayoendelea mkoani Njombe kabla ya kuahirishwa kwa mkutano wa Bunge Ijumaa Februari 8, 2019.

Ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma jana Jumatatu Februari 4, 2019 kufuatia mwongozo ulioombwa bungeni na mbunge wa Lupembe (CCM), Joram Hongole aliyetaka Bunge kuahirisha shughuli zake ili kujadili mauaji hayo.Mbunge huyo amesema taharuki imezuka mkoani Njombe na shughuli za uchumi zimesimama baada ya mauaji ya watoto chini ya miaka 10 wapatao saba.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amesema jambo hilo ni zito na serikali inajiandaa ili kutoa ripoti ya uchunguzi.Akijibu mwongozo huo, Spika Job Ndugai amesema ni jambo kubwa linalohuzunisha na kusikitisha na kuagiza kabla Bunge kuahirishwa wanataka kupata maelezo ya juu ya nini kinachoendelea mkoani humo na kisha kuangalia nini cha kufanya.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameagiza serikali kufanyia kazi kwa haraka suala la kuanzisha bima ya afya moja ili wananchi wote wapate huduma pindi wanapohitaji kama ilivyo kwa nchi ya Ghana na Rwanda.

Ndugai alitoa agizo hilo jana bungeni baada ya majibu ya serikali kuhusu mchakato wa kuanzisha bima hiyo.Awali, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alisema wizara hiyo imeandaa mapendekezo ya kuanzisha bima ya afya moja na kuwasilishwa katika ngazi mbalimbali za maamuzi serikalini.

Filed Under: Habari Kitaifa

kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na wenzake imeahirishwa.

February 1, 2019 By

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiahirisha kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake.Kesi hiyo iliyokuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye ameteuliwa kuwa Jaji, ilitajwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kevin Mhina.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza mahakama kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na wana rufaa maalum ambayo bado haijasikilizwa, hivyo wanaomba ahirisho.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi February 14, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya February Mosi na 16, mwaka huu maeneo ya Dar es Salaam.

Filed Under: Habari Kitaifa

Spika “Tumeshamlipia milioni 250 Tundu Lissu”.

February 1, 2019 By

Mkutano wa kumi na nne wa Bunge la kumi na moja umeendelea Dodoma ambapo Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amelieleza Bunge kwamba hadi sasa Ofisi yake imeshamlipia gharama za matibabu pamoja na stahiki zake Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu jumla ya shilingi Milion 250 ambapo ametoa onyo la kumtaka Mbunge huyo kuacha mara moja kuendelea kuiongopea jamii kwamba Bunge halijatoa hata senti.

Kwa upande wake Tundu Lissu katika mahojiano na chombo kimoja cha habari cha kimataifa hapo jana amesisitiza kuwa Bunge la Tanzania halijawahi kutoa hata senti moja kugharamia matibabu yake.Lissu amesema pesa hizo ni zile za michango ya wabunge pamoja stahiki zake yaani mshahara na posho kama ilivyo kwa wabunge wote

Katika hatua nyingine Wabunge wameitaka Serikali kuangalia upya adhabu zilizowekwa katika Muswada wa Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira, ikiwemo mtu atakayepatikana kwa kosa la matumizi ya mabaya ya maji kutozwa faini ya kati ya Sh5milioni hadi Sh10 milioni.Akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani bungeni  msemaji wa kambi hiyo, Hamidu Bobali amesema faini zilizowekwa katika makosa hayo ni kubwa  ukilinganisha na uzito wa kosa ambalo lingehitaji tu kuelimishwa.

Amesema kifungu cha 65 cha muswada huo kinaozungumzia makosa ya kutumia maji kinyume na matumizi yaliyoainishwa ambapo adhabu imeainishwa kuwa faini ya kiasi cha Sh5milioni au kifungo kisichopungua miezi sita.Pia amesema kifungu cha 66 cha muswada huo kimebainisha kuwa adhabu kwa makosa kama ya kuosha au kufua na kuoga na kusababisha au kuruhusu kitu kuingia kwenye miundombinu ya maji ni faini ya Sh 50,000 au isiyozidi Sh 1milioni au kifungo cha mwezi mmoja.

Filed Under: Habari Kitaifa

Wananchi mkoani Tabora kupata elimu ya sharia bule

February 1, 2019 By

Wananchi mkoani Tabora wameshauriwa kujitokeza kupata elimu ya sheria itakayowasaidia katika kutatua masuala mbalimbali yanayojitokeza katika maisha yao ya kila siku.

Hapo jana January 31 2019 ilikuwa ni siku ya kwanza katika wiki ya msaada wa kisheria Sumera Manoti mtendaji wa mahakama amezungumza na radio uhai fm ambapo amewataka wananchi kujitokeza katika viwanja vya chipkizi vilivyopo katika manispaa ya Tabora ili kupata msaada huo kutoka kwa wataalam wa sheria.

Bw Manoti  amesema kuwa katika wiki hii ya msaada wa kisheria wananchi ndiyo wadau wakuu kwani wengine hukosa haki zao za kisheria kutokana na kutofahamu utaratibu akitolea mfano wa malalamiko ya raia kutoshiriki kikamilifu kutoa ushahidi pale wanapotakiwa kufika mahakamani .

Bi Aisha Abdalah ambaye yeye ni afisa utumishi mahakama ya Tabora amesema kuwa msaada wa kisheria unaotolewa siyo tu wa kuwasaidia katika kesi mahakamani bali pia katika maisha ya kila siku nakuwa watu wamekuwa wakiogopa kufika mahakamani kupata msaada huo. Wiki ya huduma ya msaada wa kisheria imeanza janza January 31 na itahitimishwa February 6 2019 ikilenga zaidi kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao.

Filed Under: Habari Kitaifa

Waitara Amepiga Marufuku Wanafunzi Wa Shule Binafsi Ambao Hawajamaliza Ada Kusimamishwa Au Kufukuzwa Shule

January 11, 2019 By

Naibu Waziri, Ofisi Ya Rais Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara Amepiga Marufuku Wanafunzi Wa Shule Binafsi Ambao Hawajamaliza Ada Kusimamishwa Au Kufukuzwa Shule.

Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Leo, Alhamisi Januari 10, 2019, Jijini Dar Es Salaam, Waitara Amesema Kuanzia Kesho Ijumaa Ataanza Kupokea Taarifa Kutoka Kwa Katibu Tawala Wa Mikoa, Wakurugenzi Wa Halmashauri Na Wadhibiti Ubora Wa Shule Ambazo Zimewafukuza Au Kuwarudisha Wanafunzi.

Amesema Ni Marufuku Mwanafunzi Kusimamishwa Au Kufukuzwa Shule Kwa Sababu Ya Kutolipa Ada Bila Kujali Anasoma Shule Ya Umma Au Binafsi.

Waitara Amesema Jambo Jingine Ambalo Serikali Haikubaliani Nalo Ni La Wazazi Kulazimishwa Kulipa Ada Kwa Mkupuo Na Iwapo Hawajafanya Hivyo Wanafunzi Hawataendelea Na Masomo Hata Kama Mwaka Uliopita Walifanya Hivyo.

“Nina Sms (Ujumbe Mfupi Wa Maandishi) Nilizotumiwa Na Wazazi Wa Shule Ambazo Zimerudisha Wanafunzi Nyumbani Kwa Kukosa Ada Na Malipo Mengine Ya Kiholela Kama Vile Kulazimishwa Kununua Sare Za Shule Shuleni, For Figer, Rim Na Madaftari Ya Ganda Gumu (Counter Book),” Amesema Waitara.

“Nataka Maofisa Elimu, Wakurugenzi Na Makatibu Tarafa Kwenda Kwenye Hizi Shule (Anazitaja Shule) Hadi Kufikia Kesho Niwe Na Majibu Yanayoonyesha Kupatikana Ufumbuzi.”

Waitara Pia Amewataka Wazazi Ambao Watoto Wao Wamerudishwa Kwa Ajili Ya Kutolipa Au Kukamilisha Ada Wafike Kwenye Ofisi Alizozitaja Au Tamisemi Kwa Ajili Ya Kupatiwa  Ufumbuzi.

Filed Under: Habari Kitaifa

Mwalimu wa Shule ya Sekondari jijini Dodoma, amefariki dunia baada ya kunyweshwa sumu na watu wasiofahamika

January 11, 2019 By

Mwalimu Nocka Mwaisango (28) wa Shule ya Sekondari Kibwe, jijini Dodoma, amefariki dunia baada ya kunyweshwa sumu na watu wasiofahamika.Alikufa wakati akitokea mkoani Dodoma kwenda kijijini kwao mtaa wa Mtakuja, Mbalizi Wilaya ya Mbeya Vijijini kwa lengo la kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.

Baba mzazi wa mwalimu huyo, Oddy Mwaisango, alisema alipigiwa simu Desemba 20, mwaka jana na mtoto wake huyo kuwa anatarajia kwenda Mbeya kwa mapumziko ya sikukuu na kwamba atatumia mapumziko hayo kumuoa mchumba wake wa muda mrefu.

Alisema baada ya kupigwa simu hiyo, alishangaa kuona muda mrefu unapita bila kumuona na wiki moja baadaye alipigiwa simu na watu wasiofahamika waliotumia namba ya simu ya mtoto wake wakisema kuwa wanamshikilia kwa kazi maalum.

Alisema baada ya kauli hiyo aliamua kwenda Kituo cha Polisi Mbalizi, kuripoti tukio hilo.

Alisema siku iliyofuata mama yake alienda Dodoma katika shule aliyokuwa akifundisha kukutana na Mwalimu Mkuu ambaye alimjibu kuwa mtoto wake hakumuaga alipoondoka.

Alisema, ilibidi aende kuripoti Polisi Dodoma na Kitengo cha Uchunguzi wa Mawasiliano mkoani humo kiligundua kuwa mwalimu huyo yuko mkoani Morogoro.“Ilibidi mama yake asafiri hadi Morogoro na aliripoti kituo cha polisi na kukabidhiwa mtu wa uchunguzi wa mitandao ndipo katika kuchunguza wakabaini wahalifu hao na mwalimu huyo wako mkoani humo, lakini ghafla wakawa hawaonekani kwenye mtandao,” alisimulia.

Alisema baadaye wahalifu hao walimpigia simu (baba) wakihitaji Sh. 5,000,000 kama kikombozi, lakini kwa sababu hakuwa na fedha aliwatumia Sh. 500,000 ili wamwachie.

Aliongeza kuwa siku iliyofuata mtoto wake aliwapigia simu mwenyewe na kuwaambia kuwa yuko kituo cha daladala cha Tazara Mbeya na walipoenda kumfuata walikuta hajitambui.

Aidha, alisema waliamua kumkimbiza hospitali ya Ifisi iliyoko Wilaya ya Mbalizi na baadaye walimhamishia Hospitali ya Rufani Mbeya.

Alisema akiwa wodini aliongezewa maji ya kutosha, lakini alikuwa analalamika kuumizwa kwenye koo na kifuani na katika uchunguzi wa madaktari ilibainika amenyweshwa sumu.

Alisema siku iliyofuata mwalimu huyo alifariki akiwa hajawataja waliomfanyia unyama huo huku chanzo cha kifo kikitajwa kuwa ni dawa aina ya ‘Asphxia Due Mothorax’ aliyonyweshwa.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibwe, Dodoma, Mwasiti Msokola, alikiri kupata taarifa za kifo cha mwalimu wake na kwamba suala hilo linashughulikiwa na mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wake.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Filed Under: Habari Kitaifa

Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka (Hoima) Uganda hadi Mkoani Tanga haujasimama

December 10, 2018 By

Serikali imesema utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka (Hoima) Uganda hadi Mkoani Tanga haujasimama na kwamba hatua za utekelezaji wa mradi huo zinaendelea na

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani baada ya kumalizika Mkutano wa majadiliano ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba hilo uliomkutanisha na Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.

Amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo uko katika hatua nzuri na kwamba pande zote mbili wamejadiliana na kukubaliana kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa pamoja na hatua za utkelezaji za mradi.

Mradi huo utakuwa manufaa kwa jamii na makampuni ya ndani na kusisitiza bomba lina urefu kilometa 1435 huku kilometa 1115 zikiwa sehemu ya Tanzania.

Kwa upande Waziri Muloni amesema watahakikisha watafikia makubaliano na makampuni ili yaweze kusaini utekekezaji wa mradi ukamilike mwaka 2020 ilivyopangwa.

Filed Under: Habari Kitaifa

Wakulima wa korosho 82,835 Mtwara walipwa fedha zao

December 10, 2018 By

Jumla ya wakulima wa korosho 82,835 katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Lindi wamelipwa fedha zao hadi kufikia Desemba 8 mwaka huu, fedha iliyolipwa kwa wakulima hao ambao tayari wamefanyiwa uhakiki ni Bilioni 83 ambapo katika mkoa wa Mtwara wakulima 50,835 wamelipwa mkoa wa Lindi wakulima 22,131 na Mkoa wa Ruvuma ni wakulima 9,445

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo  Japhet Hasunga tarehe 9 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji wadogo wa korosho kutoka katika mikoa mitano ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Morogoro uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Mtwara.

Hasunga amesema, jumla ya vyama 328 vimefanyiwa uhakiki kati ya vyama 504 vilivyopo katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambapo jumla ya vyama 319 vimekwishalipwa.

Filed Under: Habari Kitaifa

Adakwa na Polisi kwa tuhuma za kumpa mimba bintiye

November 16, 2018 By

Polisi mkoani Arusha wanamshikilia mkazi wa Sakila, Kata ya Kikatiti, wilayani Arumeru, David Nnko (73), kwa tuhuma za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la sita (jina la mwanafunzi na shule vinahifadhiwa).Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, aliwaambia waandishi wa habari kuwa matukio ya ubakaji na utiaji mimba yamekuwa mengi wilayani humo na katika miaka miwili iliyopita, wanafunzi 84 wa shule za sekondari na msingi wamekumbwa na tatizo hilo.

Alisema kutokana na vitendo hivyo kukithiri, serikali wilayani humo imeamua kushirikiana na viongozi wa vyombo mbalimbali kukabiliana na suala hilo kwa kuunda kamati maalum.Lakini wilaya yetu tumeamua kutenga wiki nzima kuanzia Jumanne ijayo tutapokea malalamiko ya wote waliobakwa na kupatiwa mimba kwa kipindi cha miaka mitano nyuma. Hata kama kesi zao ziko mahakamani au polisi waje kutueleza ili tuongeze nguvu zichukuliwe hatua za haraka,” alisema.Alisema mbali na kupokea malalamiko hayo mbele ya kamati maalum itakayoongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, James Nchembe, pia watawaonyesha hadharani watuhumiwa wote wa ubakaji ili jamii na dunia iwafahamu.

Muro alisema wilaya hiyo imekithiri matukio hayo kila siku lazima wapokee taarifa za masuala hayo, kitendo ambacho serikali haiwezi kuvumilia.”Sisi tutawaonyesha hadharani ili wajulikane na hata wakienda mahakamani wakafanya michezo yao kumaliza kesi, jamii itakuwa imewafahamu na hii itasaidia watu wawaogope kama wabakaji,” alisema.Aidha alisema mtuhumiwa huyo alimrubuni mwanafunzi huyo amsaidie kupukuchua mahindi debe moja na akampa ‘sado’ moja kama ujira wa kazi. Alidai baada ya kazi hiyo alimvutia ndani na kumbaka.

Akizungumza mbele ya wanahabari, mkuu wa wilaya na polisi, Nnko alisema yeye si mhusika wa mimba hiyo. Alidai kuwa amesingiziwa na mwanafunzi huyo ambaye ni ndugu yake kwa sababu baba yake ni mdogo wake.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kikatiti, Amida Mnyenyelwa, alisema alipata taarifa shuleni kwa wanafunzi huyo kuhusu utoro wake na walianza kumfuatilia na wakabaini mjamzito.”Tulipobaini tulimbana akamtaja huyu mzee Nnko kuhusika na alifanya naye tendo la ndoa mara mbili na hadi kumpa mimba hiyo,” alisema.

Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Flora Nnko, alisema mtuhumiwa ni shemeji yake na alikuwa akimtuma mtoto wake kwenda kwa mtuhumiwa huyo kuchuma mchicha na kupukuchua mahindi bila hofu.”Sasa tukawa tunashangaa kuona mtoto wetu anaumwa na mume wangu alipokwenda kumpima tukabaini mjamzito wa wiki nane na tulipombana na walimu wake akamtaja huyu shemeji yangu,” alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo hana mke na anaishi mwenyewe

Filed Under: Habari Kitaifa

  • Page 1
  • Page 2
  • Page 3
  • Next Page »

Primary Sidebar

Useful Links

Swahili Christian Resources
http://www.swahilichristian.org

Bible Questions and Answers in Swahili
https://www.gotquestions.org/Kiswahili/

Listen to Swahili Christian Teaching Programs on the Internet
http://www.radiouhai.org/teachingprog.html

News Category

  • Habari Kitaifa (21)
  • Habari za Kimataifa (67)
  • Habari za Michezo (19)
  • Habari za Tanzania (19)
  • National News (11)
  • Radio (1)
  • Uncategorized (5)

Recent News

  • Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itigi ashikiliwa na Jeshi la Polisi
  • Spika wa Bunge ameiagiza Serikali kutoa kauli kuhusu mauaji ya watoto
  • Watu saba wamepoteza maisha kwa ajali ya moto jijini Paris
  • Papa Francis ahitimisha ziara yake Falme za Kiarabu
  • kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na wenzake imeahirishwa.

Follow Us

  • Facebook
  • Twitter
  • Vimeo

Watch Now!!!

http://radiouhai.co.tz/wp-content/uploads/2018/06/gmt_x264.mp4
http://radiouhai.co.tz/wp-content/uploads/2018/06/jesus-explanation_x264.mp4
http://radiouhai.co.tz/wp-content/uploads/2018/06/who-is-jesus-wrong_x264.mp4

Footer

  • Habari za Tanzania
  • Habari za Kimataifa
  • Habari za Michezo
  • Changia Redio Uhai Ukiwa nje ya Nchi
  • Changia Redio Uhai ukiwa Tanzania
  • Podcast
  • Paypal

News Category

  • Habari Kitaifa (21)
  • Habari za Kimataifa (67)
  • Habari za Michezo (19)
  • Habari za Tanzania (19)
  • National News (11)
  • Radio (1)
  • Uncategorized (5)

Follow Us

  • Facebook
  • Twitter
  • Vimeo
February 2019
M T W T F S S
« Jan    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728  

Copyright 2018: Radio Uhai