LIBYA YAFUNGA KISIMA CHA MAFUTA WAKATI MZOZO UKITOKOTA

Viongozi wa kikabila kusini mwa Libya wamekifunga kisima kikubwa zaidi cha mafuta nchini humo. Ni hatua ya karibuni kabisa ya kufungwa kisima cha mafuta wakati kukiwa na mzozo mkali kati ya serikali mbili pinzani
Viongozi wa kikabila kusini mwa Libya wamekifunga kisima kikubwa zaidi cha mafuta nchini humo. Ni hatua ya karibuni kabisa ya kufungwa kisima cha mafuta wakati kukiwa na mzozo mkali kati ya serikali mbili pinzani
Uzalishaji mafuta katika kisima cha Sharara umesitishwa na shirika la kiserikali la National Oil Corp
limetangaza amri ya Force Majeure, ambayo ni mbinu ya kisheria inayoiwezesha kampuni kuondokana na majukumu yake ya kimkataba kwa sababu ya mazingira yasiyo ya kawaida
Shirika hilo mafuta limeiita hatua ya kufungwa kisima hicho kuwa ya kipuuzi na inayoonesha mkwamo unaoendelea nchini humo. Viongozi wa kikabila katika mji wa jangwani wa Ubari, walisema walikifunga kisima hicho kulalamikia serikali ya Waziri Mkuu anayekabiliwa na mbinyo Abdul Hamid Dbeibah. Kisima cha Sharara kinazalisha karibu mapipa 450,000 kwa siku
Aprili 21, 2022
RAIS WA ZAMANI WA BOTSWANA AITWA MAHAKAMANI

Rais wa zamani wa Botswana, Ian Khama, ametakiwa kufika mbele ya mahakama mjini Gaborone kujibu makosa 13 ya jinai, likiwemo la kumiliki silaha kinyume na sheria
Hati ya wito iliyotolewa na mahakama, ambayo shirika la habari la AFP imeiona, inaonesha Khama anakabiliwa pia na makosa ya kupokea mali ya wizi na kughushi nyaraka za umiliki wa silaha
Kwa sheria ya Botswana, kumiliki bunduki kinyume na sheria kuna adhabu ya kifungo cha hadi miaka 10 gerezani.
Haijafahamika iwapo Khama, ambaye alikuwa rais wa Botwasa kwa miaka 10 hadi mnamo 2018, ataitikia wito huo wa kufika mahakamani
Katika shauri hilo, Khama, ambaye sasa anaishi nchini Afrika Kusini alikokimbilia Novemba mwaka uliopita, anashtakiwa pamoja na mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi pamoja na mkuu wa polisi aliyefutwa kazi
Aprili 21, 2022
URUSI NA UKRAINE: NI KWANINI VITA VIJAVYO VYA DONBAS MASHARIKI MWA UKRAINE VINATARAJIWA KUWA VYA UMWAGAJI DAMU NA VYA MAAMUZI

Sehemu kubwa ya vita vya mashariki mwa Ukraine vimekuwa vikipiganiwa katika maeneo ya wazi
Watu katika mashariki mwa Ukraine wanafahamu kuwa Warusi wanakaribia kuwavamia kwa mashambulizi hapa. Hata mbwa mitaani wanaonekana kujua fika, na wanaweza kusikika wakibweka kila mara kombora zito linapoaunga umbali nae neo hili
Maelfu kwa maelfu ya watu tayari wamekwishatorokea katika maeneo yenye hali ya usalama kiasi ya magharibi mwa Ukraine. Kwa mara nyingine tena msururu mrefu wa magari ya Urusi umenaswa na picha za setilaiti -mara hii ukielekea eneo la masharariki.
Katika Donbas kumeshuhudiwa dalili za Ukraine ikileta zana zaidi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na vifaru na mifumo ya ulinzi ya makombora ya masafa marefu ya anga. Lakini sio kwa kiwango cha Urusi
Ukraine inaweza kuwa inatumia mbinu zaidi katika kuwapeleka wanajeshi wake Donbas au ina wanajeshi wachache. Haijafahamika
Wengi wanaamini katika awamu ijayo ya vita katika mashariki inaweza kuamua matokeo ya mzozo huu
Aprili 18, 2022
'MPANGO WA UINGEREZA WA KUWAPELEKA WAHAMIAJI RWANDA 'NI KINYUME NA MPANGO WA MUNGU'

Askofu mkuu akiwa amebeba msalaba katika maadhimisho ya Wiki Takatifu
Mpango wa serikali wa kuwatuma baadhi ya wahamiaji kutoka Uingereza kwenda Rwanda ni "kinyume na asili ya Mungu ", Askofu Mkuu wa Canterbury alisema
Katika mahubiri yake yake ya Pasaka , Justin Welby amesema kuwa kufufuka kwa Kristo haukuwa muda wa "kuwapatia wengine majukumu yetu"
Pia ametoa wito wa usitishwaji wa mapigano nchini Ukraine ambapo alizungumzia kuhusu hofu yake juu ya gharama ya kuishi iliyotokana na mzozo.Serikali inasema mabadiliko yanahitajika kuyalinda maisha ya watu dhidi ya wasafirishaji haramu wa watu
Chini ya mpango wa pauni milioni 120-uliotangazwa wiki iliyopita - watu walioonekana kuingia Uingereza watasafirishwa vibaya katika nchi ya Afrika Mshariki, ambako wataruhusiwa kuomba haki ya kuishi
Aprili 18, 2022
VITA VYA UKRAINE: PUTIN AAPA KUENDELEZA UVAMIZI MPAKA MALENGO YAKE "MAKUU" YATIMIE

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameapa kuendeleza mashambulizi Ukraine hadi malengo ''makuu'' ya nchi yake yatimie.
Amesema mazungumzo ya amani yamefikia kikomo na kusisitiza uvamizi huo - ambao uko katika wiki yake ya sita - unaendelea kama ilivyopangwa.
Afisa wa Ukraine, hata hivyo, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mazungumzo yalikuwa magumu lakini yanaendelea
Aprili 13, 2022
MAMA YAKE OSINACHI AZUNGUMZA KWA MARA YA KWANZA

Mama na dada wa marehemu Osinachi Nwachukwu wamezungumza kwa mara ya kwanza tangu mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili alipofariki siku ya Ijumaa tarehe 2 mwezi Aprili.
Ndani ya mahojiano na mwandishi wa kujitegemea wa BBC Hyacinth Ogbu akiwa na familia ya Osinachi, wameeleza maumivu yao na kueleza kuhusu hali mbaya aliyopitia na mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu.
Bi. Madu, mama Osinachi alieleza uchungu wa tukio la mwanae.
Lakini ripoti za awali zilisema kuwa msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa akiugua saratani ya koo, lakini familia yake inakanusha hilo, ikidai kuwa alikuwa mwathirika wa unyanyasaji wa nyumbani.
Mumewe Peter Nwachukwu bado hajatoa maoni yake kuhusu shutuma hizo dhidi yake
Msemaji wa polisi alisema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo chake
Aprili 13, 2022
WAFUGAJI TURKANA WABADILI MFUMO WA MAISHA KUTOKANA NA UKAME

Makali ya ukame yamewasukuma wafugaji wa Turkana kubadili mfumo wa maisha. Uhaba wa mvua na kiangazi cha muda mrefu kimezikausha Nyasi Na maeneo ya malisho
Mji wa Lodwar umepata uhai mpya tangu serikali za ugatuzi kuzinduliwa. Biashara imenoga ila chanzo cha hilo ni tofauti. Mvua za msimu zimechelewa Na iliponyesha Mwaka uliopita zilikuwa chache. Halo hiyo ilisababisha uhaba wa Nyasi kwenye maeneo ya malisho Na maafa ya Mifugo. Ili kukabiliana Na hali wafugaji Sasa wamegeukia uvuvi kama Anavyoeleza Robert Kibunja,mkurugenzi wa idara ya uvuvi katika kaunti ya Turkana.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2020 masoko ya mifugo yalifungwa ili kuepusha maambukizi ya COVID 19 kusambaa. Hilo liliivuruga biashara ya mifugo kwa muda. Mwaka uliofuatia serikali ya Kenya ilitangaza janga la kitaifa la ukame. Mpango wa kuwasaidia wakaazi kwa chakula chao na mifugo yao iliepusha makali zaidi ya ukame anasimulia Bobby Ekadong, mkurugenzi wa idara ya biashara ya mifugo Na uzalishaji
Duru rasmi zinaeleza kuwa hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya kaskazini ya Kuanzia Loktangaber hadi Todonyang. maeneo ya Kakuma hadi Kibish hali inatisha. Lokichoggio Na Nanam kadhalika wakazi wako Hoi. Yusuf Abdullahi ni Afisa mkuu katika wizara ya ufugaji Na uvuvi kaunti ya Turkana Na anakiri kuwa
Aprili 04, 2022
UBAKAJI WA WANAWAKE BADO NI TATIZO KIVU KASKAZINI

Kuongezeka kwa visa vya ubakaji dhidi ya wanawake kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini kunawatia wasiwasi watetezezi wa haki za binadamu pamoja na baadhi ya mashirika yanayotetea haki za wanawake
Idadi ya wanawake wanaoendelea kudhalilishwa kingono imeongezeka tofauti na miaka miwili iliyopita katika eneo hilo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Gadhabu zimekuwa zikiongezeka katika baadhi ya mashirika ya kutetea haki za wanawake mashariki mwa Kongo kutokana na kuongezeka kwa visa vya ubakaji na udhalilishaji wa kingono dhidi ya wanawake katika maeneo kadhaa ya Kivu Kaskazini haswa maeneo yanayokaliwa na makundi ya waasi.
Hata hivyo, kulingana na ripoti ya shirika la AIDPROFEN linalotetea haki za wanawake, ilikadiriwa kuwa zaidi ya wanawake 20 walibakwa na wengine wasiopungua 42 walinyanyaswa kingono kwenye kipindi cha mwezi mmoja uliopita
Aprili 04, 2022