WAZIRI BASHUNGWA AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MVOMERO


Aprili 21, 2022
BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUISAIDIA ZAIDI TANZANIA KUFUFUA UCHUMI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuahidi kuisaidia Tanzania kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na madhara ya UVIKO-19 na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine
Dkt. Nchemba amesema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani
Alimweleza Kiongozi huyo kwamba Tanzania inafanya kila njia kuhakikisha kuwa uchumi wake ulioathiriwa na matukio hayo unarejea katika hali ya kawaida kwa kutafuta rasilimali fedha na kuzielekeza kwenye sekta zitakazochochea ukuaji wa uchumi ikiwemo kilimo, na kuimarisha sekta binafsi
Aprili 21, 2022
MAWAZIRI WAELEZA FAIDA YA FILAMU YA ROYAL TOUR

Viongozi wa sekta mbalimbali nchini wameeleza namna Tanzania itakavyonufaika kutokana filamu ya ‘Royal Tour’ itakayozinduliwa kesho na Rais Samia Suluhu Hassan jijini New York nchini Marekani.
Filamu ya Royal Tour iliyorekodiwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar ina lengo la kutangaza duniani vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.
Royal Tour ilianza kurekodiwa Agosti 29, 2021 na muongozaji wa filamu hiyo ni Peter Greenberg aliyeambatana na Rais Samia kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo Mji Mkongwe na hifadhi za Taifa zinazopatikana Tanzania bara
Viongozi hao wakiwemo mawaziri wa utalii wa Tanzania na Zanzibar wameeleza hayo katika mjadala uliendeshwa kwa mtandao na Watch Tanzania. Mjadala huo uliongozwa na Hezron Makundi na uliangazia maana ya Royal Tour kwa maendeleo ya Tanzania na namna itakavyonufaika
Aprili 18, 2022
VURUGU ZAZUKA KANISANI MBEYA, POLISI WAKAMATA VIONGOZI

Wakati mgogoro ukizidi kufukuta kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde, leo baadhi ya waumini wa usharika wa Mbalizi wamemzuia mchungaji wao,Atupele Mlawa kuingia kanisani na kusababisha kuvunjika kwa ibada.
Kutokana na vurugu hizo, Jeshi la Polisi mkoani humo limefika kanisani hapo na kukamata baadhi ya viongozi wa kanisa hilo
Vurugu hizo zimetokea April 17 wakati Wakristo kote duniani wakisherekea siku kuu ya Pasaka.
Baadhi ya waumini waliozungumza kanisani hapo wamesema vurugu zilianza baada ya baadhi ya wauminikufunga milango kumzuia mchungaji Mlawa kutoingia ndani kuendesha ibada wakidai kutumia vibaya mali za kanisa hilo
Taarifa zaidi zimesema waumini wanaompinga Mchungaji Mlawa, wanamtaka Mchungaji Lusajo Sanga aliyechaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi uliofanyika Machi 22 chini ya Kiongozi wa Kanisa hilo nchini, Dk Fredrick Shoo
Aprili 18, 2022
TARURA, TANROAD WAKUMBUSHWA KUWEKA MAJINA YA BARABARA ILI KURAHISISHA OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nauye amezikumbusha taasisi za TANROAD na TARURA kuweka majina ya barabara ili kurahisisha Operesheni ya Anwani za Makazi
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni hiyo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Nape amesisitiza kuwa iko hatari ya ukiritimba unaoweza kufanywa na baadhi ya watu kwa kujiita majina ya mitaa yote na barabara kwa kigezo cha kuchangia fedha za utekelezaji wa zoezi la uwekeji wa Anwani za Makazi
Ameongeza kuwa, viongozi na wananchi wanatakiwa kuwa makini katika kuweka majina ya mitaa kwa kuwa kuna wadau wanajitolea, wanachangia fedha zao lakini ni vizuri majina yawe yenye uzalendo na yanayoendana na uhalisia wa nchi yetu yakiwemo majina ya viongozi pamoja na watu mashuhuri
Aprili 13, 2022
WANAOKWAMISHA OPERESHENI YA ANWANI ZA MAKAZI KUCHUKULIWA HATUA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima kuhakikisha anawachukulia hatua wale watakaobainika kukwamisha utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika Mkoa huo
Akizungumza jijini Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi, Waziri Nape ameonesha kutokuridhishwa na kasi ya utekelezaji katika Mkoa huo unaoshika nafasi ya pili kutoka mwisho
Waziri Nape amesisitiza kuwa uwekaji wa Anwani za Makazi sio zoezi la kawaida ni operesheni maalum iliyotangazwa na Rais, ambapo kukamilika kwake kutarahisisha kufanyika kwa sensa ya watu na makazi na ufikishaji wa huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi
Aprili 13, 2022
KINAMAMA TTCL WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Kiongozi wa Wanawake Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Mercy Amani (kushoto) akikabidhi sehemu ya msaada kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Bi. Sezaria Kiwango (kulia) uliotolewa na Wafanyakazi Wanawake wa TTCL kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ya jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni juhudi za kuisaidia jamii na kuungana na Serikali kutatua changamoto za kundi hilo maalum
Aprili 04, 2022
CHANGAMOTO YA MRUNDIKANO WA TAKA MJI NJOMBE KUMALIZWA

Zaidi ya Shilingi Milioni 157 Zimetumika kununulia gari la kuzolea Taka ngumu Katika Halmashauri ya mji wa Njombe kupitia mapato ya Ndani ili kukabiliana na Changamoto ya uchafu.
Mbele ya kiongozi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa ,Afisa Mazingira wa Halmashauri ya mji wa Njombe Nelson Mlwisa Anasema hii Ni kutokana na kuwapo kwa Ongezeko la Taka Katika maeneo Mbalimbali ya mji wa Njombe.
Aprili 04, 2022